• HABARI MPYA

  Monday, August 01, 2022

  M-BET WAIPA SIMBA BILIONI 26 MIAKA MITANO


  KLABU ya Simba SC imeingia mkataba wa udhamini na kampuni ya M-Bet wenye thamani ya Sh. Bilioni 26, milioni 168 na Tsh. 5,000 kwa miaka mitano.
  Akizungumza leo wakati wa hafla ya kuutambulisha rasmi udhamini huo, Mkurugenzi wa Masoko wa M-Bet, Allen Mushi amesema kwamba "Tunaamini kama M-Bet tukishirikiana na Simba tutajitangaza ndani na nje ya Tanzania."
  Akitoa mchanganuo wa udhamini huo, Mushi amesema kwamba mwaka wa kwanza Simba watapata Sh.Bilioni 4.670, mwaka wa pili Sh. Bilioni 4.925, mwaka wa tatu Sh. Bilioni 5.205, mwaka wa nne Sh. Bilioni 5.514 na mwaka wa tano na mwaka wa tano Sh. Bilioni 5.853.
  "M-Bet ni kampuni namba moja ya michezo ya kubashiriki sasa tunashirikiana na klabu namba moja Tanzania,” amesema Mushi.
  Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Simba, Salum Abdallah Muhene amesema; “Sisi Simba ni waungwana, tunawashukuru wadhamini waliopita, sasa tuko na mdhamini mpya na tunaamini tutafanya kazi kwa karibu."
  "Tunakaribisha makampuni mengine kufanya nayo kazi sababu hii ni klabu ya watu, wasiogope tuko tayari kufanya nao kazi."
  "M-Bet mlichotaka mtakipata. Pesa ni nyingi hizi, tumieni hii nafasi kutanua biashara yenu kupitia mashabiki wetu."
  "Mimi sijawahi kuona Simba Day kama hii, imeandaliwa ikaandalika, naona kama siku haifiki. Tuje kwa wingi siku hiyo." amesema Abdallah, maarufu kama Try Again.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: M-BET WAIPA SIMBA BILIONI 26 MIAKA MITANO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top