• HABARI MPYA

  Saturday, August 07, 2021

  BRAZIL WATWAA MEDALI YA DHAHABU KATIKA SOKA OLIMPIKI

  BRAZIL imefanikiwa kutwaa Medali ya Dhahabu kwa mara ya pili mfululizo kwenye Michezo ya Olimpiki upande wa soka baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Hispania ndani ya dakika 120 Uwanja wa Nissan Jijini Yokohama.
  Dakika 90 zilimalizika timu hizo zikiwa zimefungana 1-1 Matheus Cunha akiitanguliza Brazil dakika ya 45 na ushei akimalizia kazi nzuri ya Dani Alves, kabla ya Mikel Oyarzabal kuisawazishia Hispania dakika ya 61 kwa usaidizi wa Carlos Soler – na Malcom akafunga la ushindi dakika ya 108 kwa pasi ya Antony.
  Wakati Brazil ikibeba Medali ya Dhahabu, Hispania wamechukua Fedha na Mexico iliyomaliza nafasi ya tatu baada ya kuwafunga wenyeji, Japan 3-1 jana wameondoka na Shaba.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BRAZIL WATWAA MEDALI YA DHAHABU KATIKA SOKA OLIMPIKI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top