• HABARI MPYA

  Wednesday, August 04, 2021

  YANGA SC YAMUONGEZA SHIKHALO KIKOSI CHA KOMBE LA KAGAME BAADA YA KABWILI KULIMWA KADI NYEKUNDU

  KIPA Mkenya, Farouk Shikalo ameongezwa kwenye kikosi cha Yanga kinachoshiriki michuano ya Kombe la Kagame na leo ataanza dhidi ya Atlabara.
  Hiyo inafuatia Ramadhani Kabwili kutolewa kwa kadi nyekundu kwenye mechi ya kwanza dhidi ya Nyasa Big Bullets, hivyo timu kubaki na kipa mmoja, Godfrey Magaigwa ambaye ni wa kikosi cha vijana.
  Mechi za pili za Kundi A Kombe la Kagame zinaanza leo kwa Express ya Uganda kumenyana na Nyasa Big Bullet ya Malawi Saa 10:00 jioni na Yanga dhidi ya Atlabara FC ya Sudan Kusini Saa 1:00 usiku Uwanja wa Benjamin Mkapa.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC YAMUONGEZA SHIKHALO KIKOSI CHA KOMBE LA KAGAME BAADA YA KABWILI KULIMWA KADI NYEKUNDU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top