• HABARI MPYA

  Wednesday, August 04, 2021

  SIMBA SC YAMSAJILI YUSSUF MHILU WA KAGERA SUGAR ALIYEIBULIWA YANGA SC KUANZIA TIMU YA VIJANA


  MABINGWA wa Tanzania, Simba SC wamemtambulisha mchezaji wa pili mpya kuelekea msimu ujao, safari hii mzawa, Yussuf Mhilu kutoka Kagera Sugar ya Bukoba.
  Mhilu anakuwa mchezaji wa pili kutambulishwa Simba ndani ya siku mbili mfululizo, baada ya jana kutambulishwa Mmalawi Peter Banda kutoka Nyasa Big Bullet ya kwao, naye winga.
  Mhilu ni mchezaji aliyeibukia timu ya vijana ya Yanga na akapandishwa kikosi cha kwanza kabla ya kuachwa baada ya misimu mawili ndipo akaenda Bukoba.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAMSAJILI YUSSUF MHILU WA KAGERA SUGAR ALIYEIBULIWA YANGA SC KUANZIA TIMU YA VIJANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top