• HABARI MPYA

  Wednesday, August 04, 2021

  YANGA SC YALAZIMISHWA SARE YA BILA KUFUNGANA NA ATLABARA YA SUDAN KUSINI MECHI YA KUNDI A KOMBE LA KAGAME
  WENYEJI, Yanga SC wamelazimishwa sare ya 0-0 na Sudan Kusini katika mchezo wa Kundi A Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Kombe la Kagame leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Sare hiyo ya pili mfululizo baada ya ile ya 1-1 na Nyasa Big Bullet ya Malawi inaifanya Yanga ifikishe pointi mbili tu na kuendelea kushika nafasi ya pili nyuma ya Express ya Uganda yenye pointi nne.
  Nyasa Big Bullet iliyotoa sare ya 1-1 na Express leo ina pointi mbili pia baada ya sare nyingine ya 1-1 na Yanga kwenye mchezo wa kwanza, wakati 
  Atlataba inashika mkia kwa pointi yake moja kuelekea mechi za mwisho.
  Yanga itamaliza na Express, wakati Nyasa itacheza na Atlabara katika mechi za mwisho Jumamosi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC YALAZIMISHWA SARE YA BILA KUFUNGANA NA ATLABARA YA SUDAN KUSINI MECHI YA KUNDI A KOMBE LA KAGAME Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top