• HABARI MPYA

  Jumapili, Januari 05, 2020

  MASHABIKI WA YANGA WABADILIKE ILI KUPATA UHALALI WA KULAUMU

  Na Dominick Salamba, DAR ES SALAAM
  Waswahili wanamisemo mingi ambayo ukiangalia kwa jicho la tatu ina maana sana,Wanasema Ukimpenda mkeo alafu hutaki watu wajue kama unampenda inakuwa haina maana  ni sawa na bure kwani kupenda mke ni zaidi ya kumuweka moyoni inapendeza na kuwa na maana pale utakapotafsiri hisia za moyoni mwako kuja kwenye mwonekano wa macho ya nyama na matendo pia,ambapo katika hayo hata sisi wa pembeni tutajua Yes mapenzi yapo na tunayaona...Tuachane na mahusiano turudi uku ..
  Jana tarehe 4 ilipigwa mechi ya kufungulia mwaka,Yes ilipigwa thamani ya promo iliyopigwa,magazeti yaliyoandika,viingilio na kila kilichopangwa kuhusiana na mechi kilitimia isipokuwa kitu kimoja tu ambacho nitakisema mbele..

  Uwanja ulitapika..Pongezi kwa mashabiki wa Simba ambao walifanikiwa kuibadili mechi ya jana kuwa sehemu ya furaha na picnic kwao walijaa,walipendeza,walivalia jezi zao,sura zao ziliashiria soka ni burundani..Mashabiki wa Yanga sc mnakwama wapi??
  Msimu uliopita mechi ya kwanza Timu ya Yanga ikizaniwa itaadhibiwa vikali,wachezaji na benchi la ufundi wakapambana wakiwa kama yatima ukilinganisha na umati wa simba kilichotokea ni kugawana alama kwa Simba na Yanga mechi ikaisha...
  Mechi ya marudio hali ileile ingawa Yanga alipoteza kwa bao moja la Meddie kagere bado mashabiki mliikimbia timu machoni mwenu na kuibakiza mioyoni mwenu...
  Msimu huu jana mnarudia yaleyale kwa ukubwa wa Yanga na maana ya Timu ya wananchi linapofika swala la mashabiki kuiunga mkono timu inakuwa tofauti mna matatizo gani?
  Nani amewadanganya kukaa nyumbani kutaibadili timu? hamjui kuwa wachezaji nao ni binadamu wanahitaji kutiwa moyo? mtawaacha kama yatima hadi lini? mnadhani aliyesema shabiki ni mchezaji wa 12 alikosea?
  Uwanja wa Taifa umegawanywa katika pande mbili sawa ili kutoa fursa kwa mashabiki wote wa Simba na Yanga kufurahia burudani ya soka lakini nyie mnaanza kuikataa haki yenu na kuwafanya Simba waone wao ndio wanastahili na ni aibu kuona upande wa Yanga unakaliwa na mashabiki wa simba alafu unapiga makeleke uko mimi yanga hivi uko sawa kweli?
  Mnapoteza ladha halisi ya ushindani wa mechi husika mnazidi jipoteza kwenye ramani mpira unachezwa uwanjani sio kujificha huko kwenye vibanda umiza na kupiga makelele mara nani hafai nani sijui vipi,makelele yasio na mana nendeni uwanjani,ipeni nguvu timu yenu mnahitaji kutengeneza mlingano na wenzenu Simba vinginevyo mnajipoteza wenyewe..
  Hivi mnadhani jana wachezaji wa Yanga hawakutamani uwingi na shangwe ambazo wenzao simba walikuwa wanapatiwa na mashabiki wao?au mnadhani wao ni mawe hawahitaji kutiwa nguvu?kwanini mnawafanya wajione kama yatima?mnajazana mitaani kupiga makelele tu na kutafuta wa kumpa lawama wakati mnajikimbia wenyewe..
  Badilikeni kuiga mazuri ni jambo jema sana maishani thaminini huduma na kujitoa kwa timu yenu hakuna cha kuwalipa zaidi ya kuwatia moyo na kupiga makelele ya shangwe wachezaji wenu wanapokuwa wanapambana uwanjani vinginevyo mnawakosea sana..
  Hivi jana ingetoa timu yenu imeshinda mlikuwa na uhalali kweli wa kutamba wakati mmeikimbia timu uwanjani?
  Achane kujikimbia hii Timu imeipenda wenyewe kwa dhati ya mioyo yenu,uwe shimoni,nyumbani au popote haikuondolei wewe kuumia nenda uwanjani kaishangilie timu yako,ndio mchango wako mkubwa kwa timu yako,vaa jezi yako ili kuipa mapato timu yako,mana hata usipoenda utaumia na timu itakosa pesa na hayo mazuri unayoyataka hauto yapata..
  Bora ununue jezi chapa Gsm lipa kiingilio,shangilia timu yako hata ukifungwa unakuwa umeongeza kitu kwenye timu yako tofauti na kujificha huko mtaani na kuikimbia timu ni jambo la aibu sana sana..
  Watu wa nchi mbalimbali wanafuatilia mchezo wa Simba na Yanga sasa kuweni makini isije kuwa mechi ya Simba na Yanga inakuwa kama Simba day jambo ambalo ni aibu...
  Badilikeni jitokezeni uwanjani kwenye kila mechi ya timu yenu kwa faida ya timu yenu,najua mkiamua mnaweza amueni sasa ili tuone mpambano uliokamilika kwani jana wachezaji wametupa burudani mechi imetoa matokeo ya sare ila upande wa mashabiki mmetuangusha nilitamani kuona sare nyingine huko nako ili kila upande upate kinachostahili ila kwa namna iliyokuwa jana mmewakosea wachezaji wenu,benchi la ufundi na viongozi wenu,namna ya kuomba radhi ni kuujaza uwanja kila inapocheza timu yenu.
  Mwisho  niwapongeze mashabiki waliojitokeza jana bila kujali matokeo wao walijali mapenzi yao kwa timu yao,walivaa jezi zao,hawakukubali kushindwa walipaza sauti zao bila kujali chochote ili tu kuhakikisha wachezaji  wanapata molari,ule ndio ushambiki wa kweli na wenye timu endeleeni na moyo uho na hiyo ndio maana halisi ya uwanamichezo.

  @dominicksalamba
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MASHABIKI WA YANGA WABADILIKE ILI KUPATA UHALALI WA KULAUMU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top