• HABARI MPYA

  Jumapili, Januari 05, 2020

  BARCELONA YAREJEA TENA KILELENI LA LIGA LICHA YA KULAZIMISHWA SARE

  Beki Gerard Pique akimfarji kiungo Mholanzi Frenkie de Jong baada ya kutolewa kwa kadi nyekundu kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano dakika ya 75 katika mchezo wa La Liga jana Barcelona ikilazimshwa sare ya 2-2 na wenyeji, Espanyol Uwanja wa RCDE. Mabao ya Espanyol yalifungwa na David Lopez dakika ya 23 na Wu Lei dakika ya 88, wakati ya Barcelona yalifungwa na Luis Suarez dakika ya 50 na Arturo Vidal dakika ya 59 na kwa sare hiyo, Barca inarejea kileleni La Liga kwa wastani wa mabao baada ya kufungana tena kwa pointi na Real Madrid, 40 kila timu kufuatia kucheza mechi 19 


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BARCELONA YAREJEA TENA KILELENI LA LIGA LICHA YA KULAZIMISHWA SARE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top