• HABARI MPYA

  Jumatano, Januari 01, 2020

  AZAM FC YAISHUSHIA YANGA SC NAFASI YA TATU BAADA YA KUIPIGA SINGIDA UNITED 2-1 ARUSHA

  Na Mwandishi Wetu, ARUSHA
  TIMU ya Azam FC imerejea nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji wahamiaji, Singida United Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha. 
  Kwa ushindi huo, timu hiyo ya Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na familia yake inafikisha pointi 26 katika mchezo wa 13 ikizidiwa pointi nane na mabingwa watetezi, Simba SC wanaoongoza, wakati Yanga SC sasa ni ya tatu kwa ponti zake 24 za mechi 11.
  Katika mchezo wa leo, Azam FC inayofundishwa na kocha Mromania Aristica Cioaba ilitangulia kwa bao la kiungo wake, Bryson Raphael dakika ya akimalizia kazi nzuri ya kiungo mshambuliaji, Iddi Suleiman ‘Nado’.

  Lakini mtokea benchi Frank Zacharia akaisawazishia Singida United ya kocha Mrundi Ramadhani Nswanzurimo dakika ya 63 baada ya kazi nzur ya mshambuliaji mwenzake, Six Mwasekaga.
  Hatimaye Iddi Nado akamuadhibu kocha wake wa zamani, Nswanzurimo katika klabu ya Mbeya City kwa kuifungia Azam FC bao la ushindi dakika ya 89 akimalizia pasi yaw a jina lake, Idd Kipagwile.
  Kikosi cha Singida United kilikuwa; Owen Chaima, Ramadhani Yego, Erick Emmanuel, Meshack Kibona, Daudi Mbweni, Athumani Iddi, Emmanuel Manyanda, Said Mkwazu/Fizeck Zacharia dk36, David Nartey, Six Mwasekaga na Elinywesya Sumbi/Seiri Arigumaho dk59.
  Azam FC; Mwadini Ali, Nico Wadada, Bruce Kangwa, Aggrey Morris, Yakubu Mohamed, Mudathir Yahya/Salmin Hoza dk61, Iddi Suleiman ‘Nado’, Bryson Raphael, Obrey Chirwa/Shaaban Chilunda dk55, Donald Ngoma/Paul Peter dk77 na Iddi Kipagwile.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AZAM FC YAISHUSHIA YANGA SC NAFASI YA TATU BAADA YA KUIPIGA SINGIDA UNITED 2-1 ARUSHA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top