• HABARI MPYA

  Jumamosi, Oktoba 05, 2019

  TANZANIA BARA YATWAA KOMBE LA CECAFA CHALLENGE U20 BAADA YA KUIPIGA 1-0 KENYA

  Na Mwandishi Wetu, JINJA
  TIMU ya Tanzania Bara imefanikiwa kutwaa Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati kwa vijana chini ya umri wa miaka 20, CECAFA Challenge U20 baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Kenya katika mchezo wa fainali uliofanyika Uwanja wa Njeru, Jinja nchini Uganda jioni ya leo.
  Hilo linakuwa taji la pili tu kwa Tanzania Bara kihistoria la CECAFA Challenge U20, michuano ambayo imekuwa ikifanyika kwa nadra kutokana na ukosefu wa fedha za maandalizi. Mara ya kwanza Bara ilitwaa taji hilo mwaka 1971.
  Katika mchezo wa leo, bao lililowapa taji Tanzania Bara walijifunga wenyewe Kenya dakika ya 45 kupitia kwa mchezaji wao, John Otieno Onyango.

  Ikumbukwe Kenya na Tanzania Bara inayofundishwa na kocha wa klabu ya Mtibwa Sugar, Zubery Katwila zilikuwa pamoja Kundi B na mechi baina yao ilimalizika kwa sare ya 2-2.
  katika Robo Fainali Tanzania iliwatoa wenyeji, Uganda kwa kuwachapa mabao 4-2 na kwenye Nusu Fainali iliichapa Sudan 2-1.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TANZANIA BARA YATWAA KOMBE LA CECAFA CHALLENGE U20 BAADA YA KUIPIGA 1-0 KENYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top