• HABARI MPYA

  Ijumaa, Oktoba 11, 2019

  LUKAKU AWEKA REKODI YA MABAO UBELGIJI IKIITANDIKA SAN MARINO 9-0

  Mshambuliaji Romelu Lukaku akishangilia baada ya kuweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufikisha mabao 50 Ubelgiji kufuatia kuifungia mabao mawili timu yake hiyo ya taifa dakika za 28 na 41 ikiibuka na ushindi wa 9-0 dhidi ya San Marino kwenye mchezo wa Kundi J kufuzu Euro 2020 usiku wa jana Uwanja wa Roi Baudouin mjini Brussells. Mabao mengine ya Ubelgiji yalifungwa na Nacer Chadli dakika ya 31, Cristian Brolli aliyejifunga dakika ya 35, Toby Alderweireld dakika ya 43, Youri Tielemans dakika ya 45 na ushei, Christian Benteke dakika ya 79, Yari Verschaeren kwa penalti dakika ya 84 na Timothy Castagne dakika ya 90.
  Kikosi cha Roberto Martinez kimeweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kufuzu fainali za Euro 2020 kufuatia kushinda mechi zake zote saba na kukusanya pointi 21, wakifuatiwa na Urusi wenye pointi 18 na Cyprus pointi 10 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: LUKAKU AWEKA REKODI YA MABAO UBELGIJI IKIITANDIKA SAN MARINO 9-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top