• HABARI MPYA

  Alhamisi, Oktoba 10, 2019

  TP MAZEMBE YAPANGWA KUNDI A NA AGOSTO, ZESCO NA ZAMALEK LIGI YA MABINGWA

  MABINGWA watetezi, Esperance ya Tunisia wamepangwa Kundi D pamoja na Raja Club Athletic ya Morocco, JS Kabylie ya Algeria na AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
  Mabingwa wa rekodi, Al Ahly ya Misri iliyobeba taji hilo mara nane wamepangwa pamoja na Etoile du Sahel ya Tunisia, FC Platinum ya Zimbabwe na Al Hilal ya Sudan kwenye Kundi B.
  Nao mabingwa mara tano, TP Mazembe ya DRC yenye Watanzania wawili kikosini, kiungo Ramadhani Singano 'Messi' na mshambuliaji Eliud Ambokile imewekwa Kundi A pamoja na Primeiro de Agosto ya Angola, Zesco United ya Zambia na mshindi wa jumla kati ya Zamalek ya Misri na Generation Foot ya Senegal.
  Wydad Athletic Club ya Morocco iliyofungwa katika fainali ya msimu uliopita ipo Kundi C pamoja na USMA ya Algeria, Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini na Petro Atletico ya Angola.
  Gwiji wa Misri, Ahmed Hassan alichezesha droo hiyo akisaidiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Anthony Baffoe.
  Upangwaji wa droo hiyo ulihudhuriwa pia na Makamu wa kwanza wa Rais wa CAF, Constant Omari, Katibu Mkuu wa FIFA, Fatma Samoura na Wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya mashindano ya klabu na Leseni za klabu za CAF.

  Makundi yote kwa ujumla;
  Kundi A - Primeiro de Agosto (Angola), TP Mazembe (DRC), Zesco United (Zambia), Zamalek (Misri)/Generation Foot (Senegal),
  Kundi B - Etoile du Sahel (Tunisia), FC Platinum (Zimbabwe), Al Hilal (Sudan), Al Ahly (Misri)
  Kundi C - USMA (Algeria), Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini), Petro Atletico (Angola), Wydad Athletic Club (Morocco)
  Kundi D - Raja Club Athletic (Morocco), JS Kabylie (Algeria), AS Vita (DR Congo), Esperance (Tunisia).

  Wakati huo huo, droo ya mechi za mchujo wa kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika nayo imepangwa jana. 
  Mechi za kwanza zitachezwa Oktoba 27 na za marudiano zitafuatia Novemba 3 na washindi wa jumla ndio watacheza hatua ya makundi.

  Ratiba kamili;
  Horoya (Guinea) vs Bandari (Kenya)
  Young Africans (Tanzania) vs Pyramids (Misri)
  Enyimba (Nigeria) vs TS Galaxy (Afrika Kusini)
  Zamalek (Misri)/Generation Foot (Senegal) vs ESAE (Benin)
  Asante Kotoko vs San Pedro (Ivory Coast)
  KCCA (Uganda) vs Paradou (Algeria)
  Gor Mahia (Kenya) vs DC Motema Pembe (DRC)
  UD Songo (Msumbiji) vs Bidvest Wits (Afrika Kusini)
  Elect Sport (Chad) vs Djoliba (Mali)
  Green Eagles (Zambia) vs HUSA (Morocco)
  Cano Sports (Equatorial Guinea) vs Zanaco (Zambia)
  Fosa Juniors (Madagascar) vs RS Berkane (Morocco)
  Cote d'Or (Shelisheli) vs Al Masry (Misri)
  ASC Kara (Togo) vs Rangers (Nigeria)
  FC Nouadhibou (Mauritania) vs Triangle United (Zimbabwe)
  El Nasr (Libya) vs Proline (Uganda)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TP MAZEMBE YAPANGWA KUNDI A NA AGOSTO, ZESCO NA ZAMALEK LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top