KIPAJI KINGINE KUTOKA 'CHIMBO' LILILOMUIBUA FARID MUSSA
Beki wa pembeni wa Azam FC, Gardiel Michael Mbaga (kushoto) akiwa kwenye mazoezi ya timu yake jana Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya keo dhidi ya JKT Ruvu kwenye Uwanja huo. Gardiel alipandishwa msimu uliopita kutoka akademi ya klabu hiyo, pamoja na Farid Mussa Malik ambaye kwa sasa yuko kwenye majaribio ya kucheza soka ya kulipwa Hispania
0 comments:
Post a Comment