• HABARI MPYA

    Saturday, October 04, 2014

    YAYA TOURE AWASUTA 'VIZABIZABINA', APIGA BAO MAN CITY IKISHINDA 2-0

    MWANASOKA bora wa Afrika, Yaya Toure amewajibu kwa vitendo wanaomkandia baada ya kufunga katika ushindi wa 2-0 Manchester City ikiiangusha Aston Villa Uwanja wa Villa Park.
    Yaya Toure alifunga bao hilo dakika ya 82 kabla ya Sergio Aguero kufunga la pili dakika ya 88.
    Chelsea, inayoizidi pointi mbili City kileleni mwa Ligi Kuu ya England itacheza na Arsenal kesho Uwanja wa Stamford Bridge.
    Kikosi cha Aston Villa kilikuwa: Guzan, Hutton, Senderos, Baker, Cissokho, Cleverley, Westwood, Delph, Richardson/Grealish dk71, Weimann/Benteke dk61 na N'Zogbia/Bacuna dk71.
    Man City: Hart, Zabaleta, Kompany, Mangala, Kolarov, Milner, Fernandinho/Lampard dk56, Toure, Silva/Navas dk84, Dzeko/Fernando dk64 na Aguero.
    Yaya Toure akishangilia baada ya kufunga leo
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YAYA TOURE AWASUTA 'VIZABIZABINA', APIGA BAO MAN CITY IKISHINDA 2-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top