• HABARI MPYA

    Saturday, October 11, 2014

    UBELGIJI YATIA FORA KUFUZU EURO 2016, YATANDIKA MTU 6-0

    WACHEZAJI wa sasa na wa zamani wa Ligi Kuu ya England kwa pamoja wameiwezesha Ubelgiji kupata ushindi mnono wa mabao 6-0 dhidi ya Andorra katika mchezo wa Kundi B kufuzu Euro 2016 mjini Brussels. 
    Katika mchezo wao wa kwanza wa ushindani tangu watolewe na Argentina katika Robo Fainali ya Kombe la Dunia, Ubelgiji ilipata mabao yake kupitia kwa kiungo wa zamani wa Chelsea, Kevin de Bruyne dakika ya 30 na 34, mshambuliaji wa Tottenham, Nacer Chadli dakika ya 37, kabla ya Divock Origi, ambaye atajiunga na Liverpool msimu ujao kufunga la nne dakika ya 59 na Dries Mertens kufunga la tano na la sita dakika za 65 na 68.
    Mechi nyingine za Kundi B, Wales ikiongozwa na nyota wa Real Madrid imetoa sare ya 0-0 na Bosnia-Herzegovina wakati Israel imeifunga Cyprus 2-1.  

    Kiungo wa zamani wa Chelsea, Kevin de Bruyne (kulia) akipongezwa na mchezaji wa Liverpool, Divock Origi (kushoto) baada ya kufunga kwa penalti
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: UBELGIJI YATIA FORA KUFUZU EURO 2016, YATANDIKA MTU 6-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top