• HABARI MPYA

    Saturday, October 11, 2014

    MISRI 'YAFUFUKA' KUFUZU AFCON 2015, YAILAZA 2-0 BOTSWANA...TUNISIA NA SENEGAL HAKUNA MBABE

    MABAO ya Mohamed Elneny na Mohamed Salah yameipa Misri ushindi wa 2-0 ugenini dhidi ya Botswana katika mchezo wa Kundi G kufuzu AFCON mwakani nchini Morocco uliofanyika jana usiku.
    Mafarao ambao walipoteza mechi zao mbili za kwanza za kundi hilo mbele ya Senegal na Tunisia mwezi uliopita, wamerudi barabarani baada ya ushindi huo. Timu hizo zitarudiana mjini Cairo Jumatano.
    Katika mechi nyingine za jana, Senegal na Tunisia zimetoka sare ya bila kufungana kama ilivyokuwa kwa Lesotho na Angola.
    Mechi za kufuzu AFCON zinatarajiwa kuendelea leo, Guinea ikimenyana na Ghana mjini Conakry mchezo wa kundi E, Sierra Leone na Cameroon Kundi D, 
    Uganda na Togo Kundi E, Malawi na Algeria, Ethiopia na Mali, Msumbiji na Cape Verde, Kongona Afrika Kusini, DRC na Ivory Coast, Niger na Zambia, Sudan na Nigeria na Gabon na Burkina Faso.
    Mohamed Salah ameifungia Misri jana ikiilaza 2-0 Botswana
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MISRI 'YAFUFUKA' KUFUZU AFCON 2015, YAILAZA 2-0 BOTSWANA...TUNISIA NA SENEGAL HAKUNA MBABE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top