• HABARI MPYA

    Saturday, October 18, 2014

    OSCAR, FABREGAS WAING'ARISHA CHELSEA ENGLAND

    CHELSEA imeendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya England baada ya jioni ya leo kuichapa mabao 2-1 Crystal Palace.
    Kila timu ilipoteza mchezo mmoja kwa kadi nyekundu, Chelsea Azpilicueta dakika ya 40 na Palace Delaney dakika ya 43.
    Mabao ya Chelsea leo yamefungwa na Oscar dakika ya pili na Cesc Fabregas  dakika ya 51, wakati bao pekee la Palace limefungwa na Campbell dakika ya 90.
    Kikosi cha Crystal Palace kilikuwa: Speroni, Kelly, Hangeland, Delaney, Ward, McArthur, Jedinak, Ledley, Puncheon, Campbell na Bolasie. 
    Chelsea: Courtois, Ivanovic, Terry, Cahill, Azpilicueta, Matic, Fabregas, Willian, Oscar, Hazard, Remy. 
    Fabregas leo ameifungia Chelsea ikiendeleza wimbi la ushindi Ligi Kuu ya England
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: OSCAR, FABREGAS WAING'ARISHA CHELSEA ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top