• HABARI MPYA

    Saturday, October 18, 2014

    LIGI KUU BARA YASHIKA KASI, NDANDA YAFUMULIWA 3-1 NA RUVU MTWARA, COASTAL YACHINJA TENA MKWAKWANI

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    AZAM FC na Mtibwa Sugar zinaendelea kukabana kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, sasa zote zikiwa na pointi 10 kila moja, baada ya kucheza mechi nne.
    Baada ya Mtibwa Sugar kutoka sare ya 0-0 na Polisi Uwanja wa Jamhuri, Morogoro ushindi wa 1-0 wa Azam FC dhidi ya Mbeya City umewapandisha kileleni mabingwa hao watetezi.
    Azam FC sasa wanaongoza Ligi Kuu kwa wastani wao mzuri wa mabao- licha ya kulingana kwa pointi na Mtibwa.

    Mtibwa Sugar imeporomoshwa kileleni mwa Ligi Kuu na Azam FC leo

    RMATOKEO LIGI KUU BARA MECHI ZOTE LEO

    Yanga SC 0-0 Simba SC
    Mbeya City 0-1 Azam FC
    Coastal Union 2-0 JKT Mgambo
    Ndanda FC 1-3 Ruvu Shooting
    Polisi Moro 0-0 Mtibwa Sugar
    Mechi nyingine za leo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, watani wa jadi, Simba na Yanga wametoka sare ya 0-0 wakati Ndanda FC imefungwa nyumbani mabao 3-1 na Ruvu Shooting Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.
    Coastal Union imeichapa 2-0 Mgambo JKT mabao ya Rama Salim dakika ya 29 na Kenneth Masumbuko dakika ya 89.
    Ligi Kuu itaendelea kesho kwa mchezo kati ya JKT Ruvu na wenyeji Prisons Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: LIGI KUU BARA YASHIKA KASI, NDANDA YAFUMULIWA 3-1 NA RUVU MTWARA, COASTAL YACHINJA TENA MKWAKWANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top