| Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Simba SC, Mohammed Nassor 'Steven Seagal' kulia akiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya klabu hiyo, Zacharia Hans Poppe na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji, Collins Frisch na Iddi Kajuna jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakifuatilia mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baina ya timu yao na Stand United ya Shinyanga uliomalizika kwa sare ya 1-1. Hiyo ni sare ya tatu mfululizo kwa Simba SC katika mechi zote tatu za mwanzo wa msimu na mchezo ujao watacheza na Yanga SC Oktoba 18, Uwanja wa Taifa. |
0 comments:
Post a Comment