Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
KOCHA wa Uganda, Milutin Sredojevic ‘Micho’ amemuengua kikosini mwake mshambuliji Mganda, Emmanuel Okwi baada ya kuonyesha kiwango cha chini akiichezea The Cranes dhidi ya Togo Jumamosi.
Uganda inaondoka jioni ya leo kwenda Togo kwa ajili ya mchezo wa marudiano Kundi E Kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika huko Okwi akirudishwa Dar es Salaam akaimarishe kiwango kwenye klabu yake Simba SC.
“Ndiyo, nimelazimika kufanya hivyo (kumuacha Okwi),”amesema Micho akizungumza na BIN ZUBEIRY jioni ya leo kwa simu kutoka Kampala, Uganda.
Micho pia amemuacha Nahodha wake, Andy Mwesigwa, ambaye anatumikia adhabu baada ya beki huyo wa FC Ordabasy ya Kazakhstan kufikisha kadi mbili za njano ikiwemo ya jana, Uganda ikilala 1-0 Uwanja wa Namboole.
Kikosi cha Uganda kinachoondoka leo ni, makipa; Robert Odongkara na Dennis Onyango, mabeki; Dennis Guma, Godfrey Walusimbi, Savio Kabugo, Isaac Isinde, Martin Kizza na Murushid Jjuuko, viungo ni: Tonny Mawejje, Aucho Khalid, Geoffrey 'Baba' Kizito, Brian Majweja, Kizito Luwagga na Moses Oloya, wakati washambuliaji ni Geofrey Massa (Nahodha), Daniel Sserunkuma, Yunus Sentamu na Brian Umony.
Baada ya kutemwa na Uganda, Okwi sasa atalazimika kuwahi kambi yake ya klabu yake, Simba SC nchini Afrika Kusini ambayo imejificha kujiandaa na mchezo dhidi ya watani, Yanga SC Oktoba 18, Dar es Salaam.
Okwi anaweza kuondoka pamoja na wachezaji wa Simba SC walio katika timu ya taifa, Taifa Stars mabeki Miraji Adam na Joram Mgeveke na viungo Jonas Mkude, Amri Kiemba, Said Ndemla na Haruna Chanongo. Stars inacheza na Benin jioni hii Dar es Salaam na wachezaji hao wanatarajiwa kuondoka kesho.

![]() |
| Emmanuel Okwi ametemwa kikosi cha Uganda |

.png)
0 comments:
Post a Comment