• HABARI MPYA

    Saturday, October 04, 2014

    MESSI KIZIMBANI TENA KWA KUKWEPA KULIPA KODI PAUNI MILIONI 3.4

    MWANASOKA Lionel Messi atapandoshwa tena kizimbani kwa kesi ya ukwepaji kodi baada ya Jaji kuitupilia mbali rufaa ya nyota huyo wa Barcelona nchini Hispania.
    Mshindi huyo mara nne wa Ballon d'Or (tuzo ya mwanasoka bora wa dunia) na baba yake, Jorge Messi, wanatuhumiwa kukwepa kiasi cha Pauni Milioni 3.4 cha kodi kati ya mwaka 2007 na 2009.
    Muargentina huyo anarudi katika wakati mgumu tena kwa ajili ya kesi hiyo, ambayo awali ilionekana kama angeshinda kwa urahisi- lakini Jaji wa Hispania amesema taarifa yake jana kwamba mambo ni magumu.

    Lionel Messi anakabiliwa na mashitaka ya kukwepa kodi baada ya Jaji wa Hispania kuitupilia mbali rufaa yake
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MESSI KIZIMBANI TENA KWA KUKWEPA KULIPA KODI PAUNI MILIONI 3.4 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top