GHANA imelazimishwa sare ya 1-1 na Guinea katika mechi ya Kundi E kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika mwakani nchini Morocco.
Nahodha Asamoah Gyan aliwafungia Black Stars kipindi cha kwanza dakika ya 27 kabla ya Ibrahim Traore kuisawazishia Guinea dakika ya 81.
Ghana inabaki kileleni mwa Kundi E kwa kufikisha pointi tano, wakati Uganda iliyofungwa na Togo nyumbani mjini Kampala jana, inabaki na pointi zake nne.
Bao lililoizamisha Uganda jioni ya jana lilifungwa na
Donou Kokou dakika ya 30 na matokeo hayo yanaifanya Togo ibebe pointi tatu za kwanza baada ya awali kupoteza mechi mbili, wakati Cranes inabaki na pointi zake nne.
Katika mechi nyingine za jana kufuzu AFCON ya mwakani Morocco, Gabon iliilaza 2-0 Burkina Faso, mabao ya Pierre-Emerick Aubameyang dakika ya 67 na 74 mjini Libreville, Sudan iliwafunga mabingwa watetezi, Nigeria 1-0, bao pekee la Bakri Abd Elgadir dakika ya 41.
Niger ilitoka sare ya 0-0 na Zambia, Kongo ilifungwa 2-0 nyumbani na Afrika Kusini, mabao ya Bongani Ndulula dakika ya 52 na Tokelo Anthony Rantie dakika ya 55, wakati DRC imefungwa 2-1 nyumbani na Ivory Coast. Bao la DRC lilifungwa na Cedric Mongongu dakika ya 71, wakati mabao ya Tembo yalifungwa na Wilfred Bony dakika ya 23 na Max Gradel dakika ya 83.
Msumbiji iliwafunga 2-0 Cape Verde, mabao ya Saddan Guambe dakika ya 43 na Artur Faife dakika ya 60, wakati Sierra Leone imetoka sare 0-0 na Cameroon na Ethiopia ilifungwa 2-0 nyumbani na Mali mabao ya Abdoulay Diaby dakika ya 33 na Sambou Yatabare dakika ya 60.
Malawi ilifungwa 2-0 nyumbani na Algeria mabao ya Rafik Halliche dakika ya 10 na Saphir Taider dakika ya 93. Katika mechi za juzi Senegal ilitoka 0-0 na Tunisia sawa na Lesotho na Angola, wakati Botswana ilifungwa 2-0 nyumbani na Misri mabao ya Mohamed El Nenny dakika ya 56 na Mohamed Salah dakika ya 61. Mechi za marudiano zitachezwa Jumatano zikiwa ni za kwanza katika mzunguko wa pili.

![]() |
| Ibrahim Traore aliifungia Guinea |

.png)
0 comments:
Post a Comment