• HABARI MPYA

    Monday, October 13, 2014

    BALAA JUU YA BALAA ARSENAL; WELBECK AUMIA ENKA JANA AKIICHEZEA ENGLAND

    KLABU ya Arsenal inakabiliwa na hatari ya ongezeko ya idadi ya majeruhi kufuatia mshambuliaji Danny Welbeck kuumia jana England ikishinda 1-0 dhidi ya Estonia mechi ya kufuzu Euro 2016.
    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 aliondoka uwanjani baada ya kuumia enka katika mchezo huo uliofanyika mjini Tallinn na moja kwa moja kuelekea kwenye chumba cha kubadilishia nguo akiwa na daktari wa England.
    Kocha wa Three Lions, Roy Hodgson ameondoa hofu juu ya maumivu ya Welbeck kwa kusema atakuwa fiti kurejea uwanjani wikiendi. "Sifikiri kama ni majeruhi. Ametonesha enka yake tu kidogo. Madaktari hawana hofu juu ya hilo,"amesema.

    Welbeck alitonesha enka yake mwishoni mwa mchezo wa jana wa England ikishinda 1-0 dhidi ya Estonia
    Welbeck avoids the challenge of Estonia's Martin Vunk during Sunday evening's clash
    Welbeck akimkwepa mchezaji wa Estonia, Martin Vunk jana

    Mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester United alitua Emirates kwa dau la Pauni Milioni 16 katika siku ya mwisho ya kufungwa kwa pazia la usajili, na licha ya wasiwasi wa mashabiki wa Arsenal juu yake, amefunga mabao mazuri manne ikiwemo hat-trick dhidi ya Galatasaray katika Ligi ya Mabingwa.
    Welbeck pia ameendeleza moto wa mabao timu ya taifa ya England tangu aondoke Old Trafford, akifunga mabao mawili dhidi ya Uswisi na lingine dhidi ya San Marino kabla ya jana England ikiendeleza wimbi la ushindi kwa asilimia 100 kufuzu Euro 2016.
    Tayari kocha Arsene Wenger anawakosa wachezaji 10 Arsenal ambao ni majeruhi, Mesut Ozil, Aaron Ramsey, Mikel Arteta, Olivier Giroud, Mathieu Debuchy, Serge Gnabry, Yannick Sanogo, Theo Walcott na Laurent Koscielny wakati Calum Chambers atakuwa anatumikia adhabu kweye mechi ijayo. The Gunners watamenyana na Hull City Uwanja wa Emirates Jumamosi katika mfululizo wa Ligi Kuu ya England.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BALAA JUU YA BALAA ARSENAL; WELBECK AUMIA ENKA JANA AKIICHEZEA ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top