• HABARI MPYA

    Monday, July 14, 2014

    EVRA ATHIBITISHA KUHAMIA JUVENTUS

    BEKI wa Manchester United, Patrice Evra amekubali kusaini Juventus.
    BIN ZUBEIRY inafahamu kwamba beki huyo wa kushoto amethibitisha makubaliano kwa barua pepe aliyotua akiwa mapumzikoni mjini Los Angeles, Marekani.
    United imemchukua Luke Shaw kwa dau la Pauni Milioni 30 na kufanya nafasi ya mkongwe huyo, Evra iwe finyu mbele ya kocha mpya Louis van Gaal.
    Mkongwe: Patrice Evra ataondoka Manchester United na kuhamia Italia

    United ilimfunga Mfaransa huyo kwa Mkataba mpya mapema mwaka huu, lakini sasa ipo tayari kumuuza kwa mabingwa hao wa Italia.
    Evra yupo mapumziko mjini LA baada ya kuiongoza Ufaransa hadi Robo Fainali ya Kombe la Dunia mwaka huu nchini Brazil.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: EVRA ATHIBITISHA KUHAMIA JUVENTUS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top