• HABARI MPYA

    Monday, July 14, 2014

    SCOLARI ATIMULIWA BRAZIL BAADA YA KUWA KOCHA WA KIKOSI KIBOVU ZAIDI KIHISTORIA

    KOCHA Luiz Felipe Scolari amebwaga manyanga Brazil baada ya wenyeji hao kuboronga katika Fainali za Kombe la Dunia mwaka huu, wakifungwa mabao 10 katika siku tano.
    Brazil ilifungwa na Uholanzi mabao 3-0 katika mchezo wa kuwania nafasi ya tatu ikitoka kuchapwa mabao 7-1 na Ujerumani katika Nusu Fainali Jumanne. Hata hivyo, bado haijathibitishwa, ni vyombo vya Habari Brazil vimeripiti amefukuzwa. 
    Scolari alikutana na viongozi wa Shirikisho la Soka Brazil Jumamosi usiku baada ya kipigo hicho, ambacho kiliwafanya wawe kikosi cha kwanza cha Brazil daima kufungwa nyumbani mfululizo tangu mwaka 1940.
    Ametimuliwa? Mambo yamekuwa mabaya zaidi kwa Luiz Felipe Scolari baada ya Brazil kufungwa 3-0 na Uholanzi
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SCOLARI ATIMULIWA BRAZIL BAADA YA KUWA KOCHA WA KIKOSI KIBOVU ZAIDI KIHISTORIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top