Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
TIMU ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Afrika Kusini ‘Amajimbos’ imewasili leo kwa ajili ya mechi dhidi ya wenyeji, Tanzania ‘Serengeti Boys’ Ijumaa wiki hii Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam kuanzia Saa 9:00 Alasiri.
Timu hiyo imefikia katika hoteli ya Sapphire Court, Kariakoo mjini Dar es Salaam na kesho asubuhi itafanya mazoezi Uwanja wa Karume, Jijini.
Mechi hiyo ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Vijana Afrika, itachezeshwa na marefa wa Shelisheli, Allister Barra atakayesaidiwa na Gerard Pool na Jean Joseph Felix Ernest wakati mezani atakuwa Nelson Emile Fred.
Kamisaa wa mechi hiyo atakuwa Andriamiasasoa Doda Nirimboavonjy kutoka Madagascar.
Kikosi cha Serengeti Boys chini ya kocha Hababuu Ali Omari kipo kambini kwa zaidi ya wiki mbili sasa kikijiandaa kwa mechi hiyo. Mechi ya marudiano itachezwa kati ya Agosti 1 na 3 nchini Afrika Kusini.
Kiingilio cha mechi hiyo ni sh. 2,000 tu na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametoa wito kwa mashabiki wengi kujitokeza kwenye mchezo huo Ijumaa.

![]() |
| Amajimbos wamefikia Sapphire Court Hotel Kariakoo mjini Dar es Salaam. Juu wachezaji chini makocha. |
Mechi hiyo ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Vijana Afrika, itachezeshwa na marefa wa Shelisheli, Allister Barra atakayesaidiwa na Gerard Pool na Jean Joseph Felix Ernest wakati mezani atakuwa Nelson Emile Fred.
Kamisaa wa mechi hiyo atakuwa Andriamiasasoa Doda Nirimboavonjy kutoka Madagascar.
Kikosi cha Serengeti Boys chini ya kocha Hababuu Ali Omari kipo kambini kwa zaidi ya wiki mbili sasa kikijiandaa kwa mechi hiyo. Mechi ya marudiano itachezwa kati ya Agosti 1 na 3 nchini Afrika Kusini.
Kiingilio cha mechi hiyo ni sh. 2,000 tu na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametoa wito kwa mashabiki wengi kujitokeza kwenye mchezo huo Ijumaa.

.png)
0 comments:
Post a Comment