Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
YANGA SC imeweka kambi makao makuu ya klabu yao, makutano ta mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam kujiandaa na mchezo wa marudiano Raundi ya Awali, Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Komorozine mwishoni mwa wiki.
Mabingwa hao wa Tanzania Bara leo asubuhi wamefanya mazoezi Uwanja wa Karume, Ilala, Dar es Salaam, ingawa haijafahamika kama wataendelea kuutumia Uwanja huo au la.
Ofisa Habari wa Yanga SC, Baraka Kizuguto ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, viongozi wanashughulikia safari ya Comoro kwa sasa na hadi kufika kesho itakuwa imefahamika timu itaondoka lini.
Yanga imetanguliza mguu moja Raundi ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa ambako watamenyana na mabingwa wa Afrika, Al Ahly, baada ya kushinda mabao 7-0 katika mchezo wa kwanza Jumamosi, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Maana yake sasa, Yanga inahitaji sare au kufungwa si zaidi ya mabao 6-0 ili kusonga mbele. Al Ahly ilituma Maofisa wake watatu kuja kuiangalia Yanga ikimenyana na Komorozine.
Baada ya mechi hiyo, Maofisa hao walianza kutafuta kambi ambayo timu yao itaweka watakapokuja nchini mwezi ujao na kwa bahati mbaya kwao, walienda kuomba Azam Complex, Chamazi wakakataliwa.
Uongozi wa Azam uliwanyima Ahly kambi kwa sababu hawakuwa tayari kuwasaidia wageni hao maandalizi ya kucheza na Watanzania wenzao. Mabingwa hao wa kihistoria Afrika, baada ya kukwama Complex, wakahamia Gymkhana.

![]() |
| Yanga na Komorozine wakiingia uwanjani juzi |

.png)
0 comments:
Post a Comment