• HABARI MPYA

    Monday, February 10, 2014

    CANNAVARO AFUNGUKA; “MIMI KAZI TU, SITAKI MAJUNGU”

    Na Renatus Mahima, Dar es Salaam 
    NAHODHA wa Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro' amewaambia wapenzi na wanachama wa klabu hiyo kuwa anachojali ni kazi tu na siyo maneno na majungu.
    Cannavaro alifunga bao la pili katika ushindi wa mabao 7-0 ambao Yanga iliupata katika mchezo wake wa kwanza wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya timu 'kibonde' ya Komorozine de Domoni kutoka visiwa vya Comoro juzi.
    Nyamazeni; Nadir Haroub 'Cannavaro' aliwapa ishara hii ya kuwanyamazisha mashabiki wa Yanga baada ya kufunga jana

    Akizungumza na BIN ZUBEIRY mara tu baada mechi hiyo kumazilika Uwanja wa Taifa jijini hapa juzi, Cannavaro alisema mpira wa miguu hauhitaji dharau, hivyo timu yake inapaswa kujiandaa kikamilifu kwa ajili ya mechi yao ya marudiano itakayochezwa nchini Comoro wiki mbili zijazo.
    "Nacheza kwa kujituma, lakini wakati mwingine nashangazwa na tuhuma zinazoelekezwa kwangu. Mpira hauhitaji dharau, leo (juzi) tumewafunga 7-0, lakini hatujui watajipangaje katika mechi ijayo," alisema Cannavaro.
    Nahodha huyo hakushangilia baada ya kufunga bao kwa kile kinachoelezwa kuwa pengine alikuwa anawajibu wapenzi, wanachama na baadhi viongozi wa Yanga wanaodaiwa kumtuhumu kucheza chini ya kiwango kutokana na 'uzee' katika mechi mbili zilizopita dhidi ya watani wao wa jadi, Simba walizotoka sare ya 3-3 kabla ya kufungwa 3-1.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CANNAVARO AFUNGUKA; “MIMI KAZI TU, SITAKI MAJUNGU” Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top