Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
KIUNGO wa Azam FC ambaye wakati mwingine hutumika kama beki, Himid Mao Mkami amesema kwamba wana matumaini ya kuwatoa Ferroviario de Beira ya Msumbiji katika Raundi ya Awali Kombe la Shirikisho Afrika.
Azam jana ilipata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya timu hiyo ya Msumbiji katika mchezo wa kwanza wa michuano hiyo, Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam na sasa wana jukumu la kwenda kuulinda ushindi huo mwishoni mwa wiki mjini Beira.
Mtoto wa kiungo wa zamani wa kimataifa nchini aliyewika Pamba SC ya Mwanza na Mtibwa Sugar ya Morogoro, Mao Mkami ‘Ball Dancer’, Himid hana wasiwasi Ferroviario watang’oka.
“Kweli wale jamaa ni wazuri, lakini sisi tunakwenda kuwafunga na kwao pia. Tumewaona vizuri na hatutarajii kama watakuwa na kitu kipya zaidi ya kile walichoonyesha hapa,”alisema Himid.
Aidha, Himid amewashukuru wapenzi na mashabiki wa soka waliojitokeza kwa wingi jana kuisapoti timu hiyo katika mchezo huo mgumu na akawaomba waendelee hivyo hivyo katika mechi zijazo.
Kwa upande wao, mabeki Malika Ndeule na Said Mourad nao pia wamesema wana matumaini makubwa ya kuwatoa wapinzani wao hao.
“Hawa jamaa kweli ni wazuri, wana nguvu na kasi na wanajituma sana uwanjani, yaani ni wapinzani kweli, lakini mimi nakuhakikishia hawa sisi tunakwenda kuwafunga na kwao pia,”alisema Mourad maarufu kama Mweda.
“Tunatarajia mechi ya marudiano itakuwa ngumu, lakini sisi tunacheza haya mashindano kwa mwaka wa pili sasa, tayari tuna uzoefu nayo ambao tutautumia kuwatoa wapinzani wetu,”alisema Malika.

![]() |
| Fundi wa mpira; Himid Mao akitoa pasi kitaalamu jana na chini akimtoka mchezaji wa Ferroviario |
“Kweli wale jamaa ni wazuri, lakini sisi tunakwenda kuwafunga na kwao pia. Tumewaona vizuri na hatutarajii kama watakuwa na kitu kipya zaidi ya kile walichoonyesha hapa,”alisema Himid.
Aidha, Himid amewashukuru wapenzi na mashabiki wa soka waliojitokeza kwa wingi jana kuisapoti timu hiyo katika mchezo huo mgumu na akawaomba waendelee hivyo hivyo katika mechi zijazo.
Kwa upande wao, mabeki Malika Ndeule na Said Mourad nao pia wamesema wana matumaini makubwa ya kuwatoa wapinzani wao hao.
![]() |
| Said Mourad kulia akisalimiana na mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Saidy Meckysadik kabla ya kuanza mechi ya jana. Wengine kulia kwake ni Malika Ndeule na Erasto Nyoni. |
“Hawa jamaa kweli ni wazuri, wana nguvu na kasi na wanajituma sana uwanjani, yaani ni wapinzani kweli, lakini mimi nakuhakikishia hawa sisi tunakwenda kuwafunga na kwao pia,”alisema Mourad maarufu kama Mweda.
“Tunatarajia mechi ya marudiano itakuwa ngumu, lakini sisi tunacheza haya mashindano kwa mwaka wa pili sasa, tayari tuna uzoefu nayo ambao tutautumia kuwatoa wapinzani wetu,”alisema Malika.

.png)
0 comments:
Post a Comment