• HABARI MPYA

    Tuesday, February 04, 2014

    SERENGETI WAIBUKA NA BONGE LA PROMOSHENI LA KUJISHINDIA SAFARI YA BRAZIL

    Na Princess Asia, Dar es Salaam
    KAMPUNI ya Bia ya Serengeti (SBL) imezindua promosheni ya 'Winda Safari ya Brazil na Serengeti' itakayowawezesha wateja wake kutembelea vivutio mbalimbali nchini humo Juni mwaka huu.
    Akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo uliofanyika kwenye viwanda vya kampuni hiyo vilivyopo Chang'ombe jijini Dar es Salaam  mchana huu, Mkurugenzi wa Masoko wa SBL, Eprahim Mafuru amesema wametenga zaidi ya Sh. milioni 700 kwa ajili ya zawadi kwa wateja wao watakaoshinda promosheni hiyo iliyoanza leo.

    "Wateja watatu, mmoja kila mwezi watajishindia tiketi za kwenda Brazil kutembelea vivutio mbalimbali mwezi Juni. Ziara ya kila mshindi nchini humo itagharimu Sh. milioni 25. Wateja wetu pia watajishindia iPad 20 zenye thamani ya Sh. milioni 18, dekoda 50 zenye thamani ya Sh. milioni sita na bia za bure zenye thamani ya Sh. milioni 600," amesema  Mafuru.
    Mkurugenzi huyo ambaye alikuwa amefuatana na Meneja wa Masoko wa kampuni hiyo, Allan Chonjo, amesema wateja wao watajishindia zawadi hizo kwa kutuma ujumbe mfupi wa simu (SMS) wenye namba zilizomo kwenye visibo vya bia watakazozinywa.
    "Hii ni sehemu ya kuwakumbuka wateja wetu na kuwadisha kwao sehemu ya mapato yetu," amesema Chonjo katika mkutano huo.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SERENGETI WAIBUKA NA BONGE LA PROMOSHENI LA KUJISHINDIA SAFARI YA BRAZIL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top