Na Prince Akbar, Dar es Salaam
VINARA wa msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Azam FC watawakosa nyota wao kadhaa akiwamo mshambuliaji wao hatari John Bocco 'Adebayor' katika mechi yao ya bkwanza ya Hatua ya Awali ya mashindano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Ferroviario Da Beira ya Msumbiji itakayopigwa Uwanja wa Azam Jumapili.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY kwenye ofisi za makao makuu ya Shirikisho la Soka (TFF) zilizopo Karume jijini Dar es Salam leo mchana, msemaji wa Azam FC, Jaffar Idd Maganga amesema watawakosa wachezaji hao katika mchezo huo muhimu kutoka na majeraha yanayowakabili.
Aliwataja wakali hao kuwa ni Ismail Lugambo ambaye Jumapili alivunjika mguu katika mechi ya kirafiki ya timu za U20 za Azam FC na Ashanti United na winga aliyechangia kuiua Yanga katika ushindi wa 3-2 msimu huu Farid Musa ambaye amekuwa akisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara na itabidi afanyiwe vipimo vikubwa.
Wengine ni Hajji Nuhu ambaye jana alianguka ghafla katika maeneo ya makao makuu ya Azam FC yaliyopo Chamazi jijini Dar es Salaam na kuumia goti lake ambalo limeshafanyiwa upasuaji mara mbili na itabidi arudishe India tena kwa ajili ya matibabu.
"Farid itabidi afanyiwe vipimo vya MRY kwenye mgongo ili tujue sababu ya kuumia mara kwa mara, Bocco bado hali ya goti lake haiko sawa. Alipewa mapumziko ya wiki mbili na tayari ameshamaliza wiki moja lakini hatacheza mchezo huo," amesema Jaffar.
"Tumejiandaa vizuri kwa ajili ya mechi hiyo dhidi ya timu ya Msumbuji. Kikosi chetu ambacho mpaka sasa hakijafungwa hata mechi moja ya ligi kuu kimebadilika sana. Tumeifunga mabao manne timu ngumu ya Kagera Sugar ambayo imekuwa ikifanya vizuri katika ligi kuu.
"Ni jambo jema mechi ijayo tunacheza kwenye uwanja wetu wa nyumbani kwa sababu tayari CAF (Shirikisho la Soka barani Afrika) wameshaidhinisha Uwanja wa Chamazi utumike kwa ajili ya mechi za kimataifa baada ya kufanyiwa uikarabati mkubwa. Tunawakaribisha wapenzi wa soka Chamazi Jumapili wafike kwa wingi," amefafanua zaidi Jaffar.
Azam, ambao msimu uliopita pia waliiwakilisha Tanzania katika mashindano hayo baada ya kumaliza wa pili ligi kuu, wakifanikiwa kuitoa Ferroviario watamenyana na mshindi kati ya St. Michel ya Shelisheli na ASSM Elgeco Plus ya Madagacar.
VINARA wa msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Azam FC watawakosa nyota wao kadhaa akiwamo mshambuliaji wao hatari John Bocco 'Adebayor' katika mechi yao ya bkwanza ya Hatua ya Awali ya mashindano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Ferroviario Da Beira ya Msumbiji itakayopigwa Uwanja wa Azam Jumapili.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY kwenye ofisi za makao makuu ya Shirikisho la Soka (TFF) zilizopo Karume jijini Dar es Salam leo mchana, msemaji wa Azam FC, Jaffar Idd Maganga amesema watawakosa wachezaji hao katika mchezo huo muhimu kutoka na majeraha yanayowakabili.
![]() |
| Azam inakabiliwa na majeruhi kadhaa |
Wengine ni Hajji Nuhu ambaye jana alianguka ghafla katika maeneo ya makao makuu ya Azam FC yaliyopo Chamazi jijini Dar es Salaam na kuumia goti lake ambalo limeshafanyiwa upasuaji mara mbili na itabidi arudishe India tena kwa ajili ya matibabu.
"Farid itabidi afanyiwe vipimo vya MRY kwenye mgongo ili tujue sababu ya kuumia mara kwa mara, Bocco bado hali ya goti lake haiko sawa. Alipewa mapumziko ya wiki mbili na tayari ameshamaliza wiki moja lakini hatacheza mchezo huo," amesema Jaffar.
"Tumejiandaa vizuri kwa ajili ya mechi hiyo dhidi ya timu ya Msumbuji. Kikosi chetu ambacho mpaka sasa hakijafungwa hata mechi moja ya ligi kuu kimebadilika sana. Tumeifunga mabao manne timu ngumu ya Kagera Sugar ambayo imekuwa ikifanya vizuri katika ligi kuu.
"Ni jambo jema mechi ijayo tunacheza kwenye uwanja wetu wa nyumbani kwa sababu tayari CAF (Shirikisho la Soka barani Afrika) wameshaidhinisha Uwanja wa Chamazi utumike kwa ajili ya mechi za kimataifa baada ya kufanyiwa uikarabati mkubwa. Tunawakaribisha wapenzi wa soka Chamazi Jumapili wafike kwa wingi," amefafanua zaidi Jaffar.
Azam, ambao msimu uliopita pia waliiwakilisha Tanzania katika mashindano hayo baada ya kumaliza wa pili ligi kuu, wakifanikiwa kuitoa Ferroviario watamenyana na mshindi kati ya St. Michel ya Shelisheli na ASSM Elgeco Plus ya Madagacar.

.png)
0 comments:
Post a Comment