• HABARI MPYA

    Monday, February 10, 2014

    MESSI AIREJESHA KILELENI BARCELONA...KITI CHA LA LIGA MWAKA HUU NI MOTO, HAKIKALIKI

    BARCELONA ya Hispania imerejea kileleni mwa La Liga kufuatia ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Sevilla ugenini jana.
    Shukrani kwao wafungaji wa mabao hayo, Sanchez dakika ya 34, Messi aliyefunga mawili dakika ya 44 na 55 na Fabregas dakika ya 87, wakati bao pekee la Sevilla lilifungwa na Moreno dakika ya 15.
    Kwa matokeo hayo, Barca inatimiza pointi 57 sawa na Real Madrid na Atletico Madrid baada ya timu zote kucheza mechi 23, lakini zinapishana kwa wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa.
    Barca ina mabao 46 zaidi, Real 41 na Atleitco 40- hii inamaanisha mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Hispania mwaka huu ni moto.
    Ushindi kwenye mvua: Lionel Messi amefunga mabao mawili jana Barcelona ikishinda 4-1 dhidi ya SevillaAt the double: Messi (left) scored twice to help Barcelona to a 3-1 win against Sevilla
    Messi (kushoto) akishangilia bao lake la pili jana
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MESSI AIREJESHA KILELENI BARCELONA...KITI CHA LA LIGA MWAKA HUU NI MOTO, HAKIKALIKI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top