• HABARI MPYA

    Sunday, February 09, 2014

    AZAM FC NA FERROVIARIO ILIKUWA SHUGHULI PEVU LEO CHAMAZI HADI KUSHINDA

    Beki wa Ferroviario de Beira ya Maumbiji, Edson Morais kushoto akimdhibiti mshambuliaji wa Azam FC kutoka Ivory Coast, Kipre Tchetche katika mchezo wa kwanza Raundi ya Awali Kombe la Shirikisho Afrika jioni ya leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam. Azam ilishinda bao 1-0 lililofungwa na Kipre Tchetche na sasa itahitaji sare katika mchezo wa marudiano wiki ijayo mjini Beira ili kusonga mbele.
    Beki wa Ferroviario, Abrao Cufa akiwania mpira dhidi ya mshambuliaji wa Azam FC, Mganda Brian Umony
    Beki wa Azam FC, Malika Ndeula hapa alifanikiwa kuruka kwanja la beki wa Ferroviario, Edson Morais na kupiga krosi
    Kipre Tchetche hapa alimpiga chenga kali beki huyu wa Ferroviario, Abrao Cufa
    Kipre Tchetche akiwatoka mabeki wa Ferroviario
    Mshambuliaji wa Azam FC, John Bocco 'Adebayor' kushoto akitafuta mbinu za kumtoka Edson Morais wa Ferroviario
    Kiungo wa Ferroviario, Manuel Fernandes na Himid Mao wa Azam kulia
    Mashabiki wa Azam kwa raha zao
    Walikuwepo; Wachezaji Shomary Kapombe wa AC Cannes ya Ufaransa kulia na Mrisho Ngassa wa Yanga SC nyuma yake walikuwepo leo Chamazi
    Walikuwepo pia; Wachezaji wa Yanga SC, kutoka kulia kipa Juma Kaseja na washambuliaji Waganda Emmanuel Okwi na Hamisi Kiiza walikuwepo leo Chamazi
    Kikosi cha ushindi; Kikosi cha kwanza cha Azam leo
    Wapinzani wagumu; Kikosi cha kwanza cha Ferroviario de Beira leo

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC NA FERROVIARIO ILIKUWA SHUGHULI PEVU LEO CHAMAZI HADI KUSHINDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top