SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) lipo katika mchakato wa kusaka mwalimu mpya wa timu za vijana pamoja na wasaidizi wake, baada ya kumsitishia ajira, aliyekuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mdenmark, Jacob Michelsen.
Hakika ni wazo, zuri kwa sababu Michelsen kama ilivyo kwa Mdenmark mwenzake, aliyekuwa kocha wa timu ya kwanza ya taifa, Taifa Stars, Kim Poulsen wameshindwa kuiletea mafanikio nchi yetu katika kipindi chote cha kufanya kwao kazi nchini (zaidi ya miaka miwili).
Lakini kumekuwa na tatizo kwa viongozi wetu wa soka, wanapoingia kwenye mchakato wa kusaka walimu, hutafuta watu wa bei rahisi bila kuzingatia uwezo wao katika utendaji wa kazi.
Hivi karibuni nilikuwa ninazungumza na kiongozi wa klabu moja nguli nchini na kumdadisi juu ya mwalimu wa kigeni waliyemchukua, nikamuuliza kweli dunia nzima huyo ndiye kocha waliyeona bora?
Nikamuambia mbona kuna makocha wengi wazuri wenye rekodi nzuri na uzoefu wa kufanya kazi Afrika ambao kwa sasa hawana kazi, kwa nini msichukue miongoni mwao hao?
Akaniambia ni kweli, lakini walimu wengi wazuri wanataka fedha nyingi, ambazo wao wanaona hawana uwezo wa kuwalipa.
Nikamuambia hamuoni kwamba huyo mwalimu wa bei poa mnayemchukua atawapotezea muda kwa kuwa si mwalimu wa uhakika, akaniambia niachane na hiyo mada nami nikaachana naye.
Lakini ukweli ni kwamba aliniacha na maswali mengi sana juu ya mustakabali wa klabu yao na soka ya Tanzania kwa ujumla kama tunapotafuta mwalimu, hatuangalii ubora, tunaangalia unafuu wa malipo yake.
Ina maana kwetu makocha wa Kizungu tunawachukua kama fasheni tu, timu ina kocha mzungu, lakini kumbe ‘fundi bomba’ na hana ujuzi wa soka- na kama hivyo ndivyo kuna ajabu gani hatuna mafanikio.
Lakini ipo haja ya watu waliopewa dhamana ya kuongoza soka yetu kulitazama zaidi ya mara moja suala la makocha na si kulichukulia kimzaha mzaha.
Makocha ambao si wa uhakika wamekwishatupotezea muda sana na hakuna haja tena ya kuendelea kupoteza muda, bali tufikirie namna ya kufikia mafanikio yaliyofikiwa na wenzetu.
Hivi sasa TFF wapo katika mchakato wa kusaka kocha wa timu za vijana na bila shaka muda si mrefu wataingia kwenye mchakato wa kusaka kocha wa Taifa Stars.
Ni vyema sana TFF wakatoa kipaumbele katika suala la ubora wa mwalimu kuliko unafuu wa bei yake- kama kweli wanataka kutuletea kocha ambaye ataleta mapinduzi ya kweli katika soka yetu.
Niwapongeze Azam FC, wamemuajiri kocha Mcameroon Joseph Marius Omog ambaye rekodi yake ni nzuri, kuanzia kwenye uzoefu wa kufanya kazi Afrika na kushinda mataji ya Afrika pia.
Naamini Azam hawakungalia gharama za mwalimu, bali walitazama bora na hiyo ni kwa sababu kuna kitu wanakitaka na kwa mwendo wao, muda si mrefu watakipata.
Lakini hawa viongozi wa klabu nyingine wanaoendekeza ubabaishaji na usanii mwingi, wataendelea kuzipotezea muda klabu zao na kuwakosesha raha mashabiki wa timu hizo.
Haitakuwa vyema TFF nayo ikafikiria ni bora mwalimu wa gharama nafuu, bila kujali uwezo wake. TFF ifanye mchakato makini katika kusaka walimu wa timu za taifa mwisho wa siku tuletewe watu ambao wataleta tija katika soka yetu.
Lazima tutambue mafanikio si jambo jepesi na kuwekeza maana yake ni pamoja na fedha katika kuziandaa timu, ambazo ni pamoja na hizo za kulipa makocha, kambi nzuri na kadhalika.
Naamini kabisa, rais mpya wa TFF, Jamal Malinzi ni mtu mwenye nia ya kweli ya kuleta mapinduzi katika soka ya Tanzania sitarajii tena kama timu zetu za taifa zitaendelea kuwa sehemu ya watu kuja kujifunzia kazi ya ukocha.
Tunataka makocha, ambao tangu huko walipotoka ni makocha na wamefanya kazi kiasi cha kutosha na rekodi zao nzuri ziwe sababu za kuajiriwa kwao. Jumatano njema.

.png)
0 comments:
Post a Comment