• HABARI MPYA

    Sunday, February 09, 2014

    KOCHA WA VIBONDE YANGA ASEMA, KILE KIPIGO KWAO SAWA TU, WANA NINI WAO!

    Na Renatus Mahima, Dar es Salaam
    BAADA ya timu yake kukumbana na kichapo kikali cha mabao 7-0 kutoka kwa Yanga leo, Kocha wa Komorozine de Domoni, In-Yadhuddine Ben amesema walistahili kipigo hicho kwa vile soka la kwao Comoro liko chini ukilinganisha na Tanzania.
    Yanga wameanza vyema hatua ya awali ya mashindano ya Klabu Bingwa Afrika baada ya kuiadabisha timu hiyo kutoka Visiwa vya Comoro idadi hiyo ya mabao Uwanja wa Taifa jijini hapa muda mfupi uliopiata. Shukrani klawea mabao ya winga hatari Mrisho Ngasa aliyepiga hat-trick, nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na mshambuliaji Mganda Hamis Kiiza waliofunga moja kila mmoja na mshambuliaji Mrundi Didier Kavumbagu aliyefunga mawili.
    Kocha wa Komorozine, In-Yadhuddine Ben 

    Akizungumza na waandishi wa habari jana baada ya mechi hiyo, Ben amesema Yanga ni timu kubwa, hivyo hana sababu ya kuwalaumu wachezaji wake kwa kukubali kipigo hicho.
    “Sijashangazwa na matokeo haya kwa sababu Yanga ni timu bora na kubwa barani Afrika. Pia soka la kwetu (Comoro) liko chini sana ukilinganisha na Tanzania ambako mpira vwa miguu unachukuliwa kama ajira,” amesema kocha huyo ambaye timu yake itarudiana na Yanga wiki mbili zijazo nchini Comoro.
    “Mpira ni mchezo wa makosa, tusubiri tuone tunafanya nini katika mechi yetu ya marudiano. Huwezi kujua, yawezekana tukashinda,” alisema zaidi kocha huyo.
    Kwa upande wake kocha wa Yanga, Mholanzi Hans van der Pluijm amesema soka ni mchezo wa makosa, ndio maana vijana wake wameyatumia makosa mengi yaliyofanywa na wachezaji wa Komorozine kupata magaoli hayo saba.
    Amesema timu yake ilikuwa na uwezo wa kupata mabao menmgi zaidi hasa kipindi cha pili lakini washambuliaji wake hawakuzitumia.
    “Tulikuwa na uwezo wa kuwafunga wapinzani yetu mabao mengi zaidi kipindi cha kwanza lakini wachezaji wetu kidogo hawakuwa sawa. Tulipoingia vyumbani wakati wa ,mapumziko tuliwaeleza bwachezaji wetu wakabadilika sana kipindi cha pili,” amesema Pluijm aliyejiunga na Yanga baada ya kutimuliwa kwa Mholanzi mwenzake Ernie Brandts Desemba mwaka jana.
    Kwa ushindi huo, Yanga imetanguliza mguu mmoja kukabiliana na mabingwa wa Afrika, Al Ahly katika hatua ya pili ya mashindano hayo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KOCHA WA VIBONDE YANGA ASEMA, KILE KIPIGO KWAO SAWA TU, WANA NINI WAO! Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top