• HABARI MPYA

    Monday, November 18, 2013

    SEIF MAGARI WA YANGA MAWINDONI KARUME, UDENDA WAMTOKA KWA MAKINDA YA SIMBA, NDEMLA...

    Hivi huyu Ndemla ana mkataba kweli Simba? Kigogo wa masuala ya Usajili ya klabu ya Yanga, Seif Ahmed Magari 'Tishio la Jiji' kulia akijadiliana jambo na Kocha wa zamani wa klabu hiyo, ambaye kwa sasa ni Mwandishi wa makala za michezo na mchambuzi wa mechi, Kenny Mwaisabula kushoto wakati wa mechi ya timu za vijana chini ya umri wa miaka 20 za Simba na JKT Oljoro jioni ya leo Uwanja wa Karume, Dar es Salaam. Seif alionekana kuvutiwa sana na uwezo wa wachezaji wa Simba SC, akiwemo kiungo Said Ndemla, anayepasua katikati ya wachezaji wa Oljoro picha ya chini. 


    Itafaa sana akicheza na Dilunga (Hassan) huyu pale katikati (Yanga); Seif akiendelea kujadiliana na Mwaisabula

    Hiyo kazi mpe huyu anakaa naye mtaa mmoja; Hapa ameongezeka kocha mwingine na mchambuzi wa mechi, John Kanakamfumu kulia

    Wewe Bin Zubeiry wewee...ntaku...; Seif akimnyooshea kidole mpiga picha hii baada ya kugundua anamchukua picha wakati anawasili Uwanja wa Karume

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SEIF MAGARI WA YANGA MAWINDONI KARUME, UDENDA WAMTOKA KWA MAKINDA YA SIMBA, NDEMLA... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top