• HABARI MPYA

  Alhamisi, Novemba 28, 2013

  DILUNGA: NI WAKATI WANGU SASA

  Na Mahmoud Zubeiry, Nairobi
  KIUNGO chipukizi wa timu ya taifa ya Bara, Kilimanjaro Stars, Hassan Dilunga amesema kwamba anataka kucheza kwa bidii katika Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge ili kujitengenezea mazingira ya kuwa na namba ya kudumu kikosini.
  Kiungo huyo wa Ruvu Shooting aliyesaini Yanga SC kwa ajili ya dirisha dogo amesema kwamba ni fursa nzuri sasa kwake kuonyesha uwezo katika mashindano haya ili kuwafurahisha wapenzi wa timu.
  Wakati wangu sasa; Hassan Dilunga amesema anataka kucheza kwa bidii ajihakikishie namba ya kudumu Stars

  “Kiu yangu ya muda mrefu kwanza ni kuwa na namba ya kudumu katika kikosi cha Taifa Stars na kupewa nafasi hapa timu ya Bara ni mwanzo mzuri wa kuelekea huko. Nataka niitumie nafasi hii vizuri, ili nitimize ndoto zangu za kuche Ulaya,”alisema.
  Mchezaji huyo amesema kwamba Tanzania kwa sasa ina viungo wengi bora na ili kukabiliana na changamoto hiyo, anapaswa kufanya kazi nzuri ya kupendeza.
  “Hii itakuwa mara yangu ya kwanza kucheza Challenge, lakini sina wasiwasi na niko vizuri tu kutokana na jinsi nilivyoandaliwa kuanzia kwenye mchezo dhidi ya Zimbabwe na ninajiona niko trayari sana,”alisema. 
  Kili Stars inatarajiwa kuanza kampeni zake za kuwania taji la nne la Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge leo kwa kumenyana na Zambia Uwanja wa Machakos katika mchezo wa Kundi B utakaotanguliwa na mechi nyingine kati ya Somalia na Burundi.         
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: DILUNGA: NI WAKATI WANGU SASA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top