• HABARI MPYA

    Thursday, November 28, 2013

    TANZANIA YAKWEA MATAWI YA JUU FIFA, HISPANIA BADO NAMBA MOJA…IVORY COAST NDIO BABA WA KANDANDA AFRIKA

    Na Prince Akbar, Dar es Salaam
    TANZANIA imepanda kwa nafasi tatu katika chati za ubora wa viwango vya soka vya FIFA kutoka nafasi ya 127 hadi nafasi ya 124. 
    Lakini Tanzania inazidiwia na nchi kibao za Afrika Mashariki na Kati, zikiwemo Kenya iliyo nafasi ya 117, Burundi 112, Ethiopia 93 na Uganda 86. 
    Sudan iliyo nafasi ya 130 ni kati ya nchi zinazofungwa tela na Tanzania katika renki hizo.
    Mchezo wa mwisho wa kimataifa wa Tanzania ilitoka sare ya bila kufungana na Zimbabwe mwezi huu

    Hispania inaendelea kushika namba moja kwa ubora wa soka duniani, ikifuatiwa na Ujerumani, Argentina na Colombia wakati Ureno sasa inashika nafasi ya tano, Uruguay ya sita, Italia ya saba, Uswisi ya nane, Uholanzi ya tisa na Brazil ya 10.
    Ivory Coast inashika nafasi ya 17 na hiyo ndiyo nchi inayoongoza kisoka Afrika, ikifuatiwa na Ghana nafasi ya 24 na Algeria 26. 

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TANZANIA YAKWEA MATAWI YA JUU FIFA, HISPANIA BADO NAMBA MOJA…IVORY COAST NDIO BABA WA KANDANDA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top