• HABARI MPYA

  Ijumaa, Novemba 29, 2013

  UGANDA YAWAFUNGA RWANDA 1-0, SUDAN YAIFUMUA ERITREA 3-0

  Na Mahmoud Zubeiry, Nairobi
  BAO pekee la Dan Sserunkuma dakika ya 88, limeipa Uganda, The Cranes ushindi wa 1-0 dhidi ya Rwanda, Amavubi katika mchezo wa Kundi C Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge 2013 Uwanja wa Nyayo, Nairobi jioni hii.
  Rwanda ilitawala sehemu kubwa ya mchezo na kukosa mabao mengi, lakini mwishoni mwa mchezo ikawaruhusu Uganda kuondoka na pointi tatu.
  Ibrahim Salah wa Sudan akimiliki mpira mbele ya Tesmafikel Suarfael wa Eritrea leo Machakos

  Wachezaji wote wa Yanga, Hamisi Kiiza alicheza upande wa Uganda na Haruna Niyonzima upande wa Rwanda.  
  Katika mchezo wa kwanza, Sudan iliifunga mabao 3-0 Eritrea kwenye Uwanja wa Kenyatta, Machakos, Salah Ibrahim akifunga mawili na moja Tahir Mohammed
  Baada ya kukamilisha mechi za kwanza za makundi, mechi za pili zitaanza kesho Ethiopia ikimenyana na Zanzibar na Sudan Kusini na Kenya, hiyo ikiwa michezo ya Kundi A Uwanja wa Nyayo.
  Katika mechi za kwanza za kundi hilo, Zanzibar iliifunga Sudan Kusini 2-1 na Kenya ilitoka sare ya bila kufungana na Ethiopia. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: UGANDA YAWAFUNGA RWANDA 1-0, SUDAN YAIFUMUA ERITREA 3-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top