• HABARI MPYA

  Alhamisi, Novemba 28, 2013

  MICHO AIPA 5 BIN ZUBEIRY…ASEMA INASAIDIA SANA SOKA YA CECAFA

  Na Zaituni Kibwana, Nairobi
  KOCHA Mkuu wa Uganda, Mserbia Milutin Sredojevic ‘Micho’ ameipongeza blogu ya BIN ZUBEIRY (bongostaz.blogspot.com) kuwa kupromoti soka ya Afrika Mashariki na Kati na akasema ni mfano wa kuigwa.
  Akizungumza jana Uwanja wa Nyayo, Nairobi, Kenya, kocha huyo wa zamani wa Rwanda na klabu za Orlando Pirates ya Afrika Kusini, St George ya Ethiopia, El Hilal ya Sudan, Yanga ya Tanzania na SC Villa ya Uganda alisema amekuwa akiifuatilia sana blogu hiyo na imekuwa ikisuuza nafasi yake.
  Sikosi kuingia ha siku moja; Kocha Micho ameisifu BIN ZUBEIRY Blog kwa kazi nzuri ya kupromoti soka ya ukanda wa CECAFA 

  “Nafuatilia sana unachokifanya, kwa kweli nakupongeza sana, wewe ni mtu muhimu sana kwa soka ya ukanda huu, na si mimi tu, watu wengi ninaozungumza nao kwa kweli wanavutiwa sana na unachokifanya,” alisema akizungumza na Ofisa Mtendaji Mkuu wa BIN ZUBEIRY Blog, Mahmoud Zubeiry.
  Micho alisema kwa sasa BIN ZUBEIRY ndiyo chanzo kikuu cha habari za Tanzania na zinazohusu mashindano ya CECAFA. “Sipati tabu tena kujua maendeleo ya wachezaji wangu wanaocheza Tanzania, BIN ZUBERY inanisaidia sana,”alisema.
  Mtendaji Mkuu wa BIN ZUBEIRY Blog, Mahmoud Zubeiry kushoto akizungumza na Mjumbe mkongwe wa CECAFA na rais wa zamani wa TFF (Tanzania), Alhaj Muhiddin Ndolanga katika hoteli ya Hill Pack 

  BIN ZUBEIRY ni blogu iliyoanzishwa rasmi Mei mwaka jana na mwandishi mwandamizi wa habari za michezo Tanzania, Mahmoud Zubeiry aliyewahi kuwa Mhariri wa gazeti kongwe la michezo nchini humo, Dimba. Blogu hiyo nambari moja Tanzania inafadhiliwa na kampuni za Bakhresa Group, Sapphire Court Hotel na ZH Poppe na pia inavutia wadau na makampuni mengine makubwa kutangaza biashara zao.
  Kwa sasa BIN ZUBEIRY imeelekeza nguvu zake katika mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge yaliyoanza jana mjini Nairobi ikiwa imepeleka wawakilishi wake wawili, akiwemo Mtendaji wake Mkuu, Mahmoud Zubeiry.         
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MICHO AIPA 5 BIN ZUBEIRY…ASEMA INASAIDIA SANA SOKA YA CECAFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top