• HABARI MPYA

  Ijumaa, Novemba 29, 2013

  NI YANGA NA COASTAL FAINALI KOMBE LA UHAI 2013

  YANGA SC imefanikiwa kuingia Fainali ya michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 20 kwa klabu za Ligi Kuu ya Bara, maarufu kama Kombe la Uhai, baada ya kuifunga Mtibwa Sugar mabao 3-1 kwenye Uwanja wa Azam Complex jioni hii.
  Mtibwa walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 14, mfungaji Shiza Kichuya na Yanga wakasawazisha kupitia kwa Notikel Masasi dakika ya 17 ambaye pia alifunga la pili dakika ya 32 kabla ya na Hamisi Issa kufunga la tatu dakika ya 86.
  Yanga sasa itamenyana na Coastal Union iliyowatoa waliokuwa mabingwa watetezi, Azam FC jana kwa kuwafunga 1-0 katika fainali Jumapili kwenye Uwanja huo huo wa Azam Complex.
  Katika hatua ya makundi, Yanga iliifunga 2-1 Coastal Union, je fainali mambo yatakuwaje?
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NI YANGA NA COASTAL FAINALI KOMBE LA UHAI 2013 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top