• HABARI MPYA

  Alhamisi, Novemba 28, 2013

  BURUNDI YAILAZA SOMALIA 2-0 MACHAKOS

  Na Mahmoud Zubeiry, Machakos
  TIMU ya taifa ya Burundi imeanza vyema michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge baada ya kuichapa Somalia mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Kenyatta, Machakos nchini Kenya.
  Mabao ya Burundi yalifungwa na Abdoul Fiston dakika ya 40 na Nduwarugira Christopher dakika ya 55.
  Mchezo wa pili wa Kundi B unatarajiwa kufanyika jioni hii kati ya Bara na Zambia kwenye Uwanja huo huo.
  Mpira ukimpita kipa wa Somalia, Mohammed Sherrif kuelekea nyavuni baada ya Abdoul Fiston kuipatia Burundi bao la kwanza leo Uwanja wa Kenyatta. 

  Burundi; Arakaza Arthur, Hakizimana Hassan, Hakizimana Pascal, Nduwarugira Christopher, Nsambyumva Frederic, Ndikumana Yussuf, Habonimana Celestin, Duhayindavyi Gael, Abdoul Fiston na Hakizimana Issa.
  Somalia; Mohamed Sherif, Hassan Ali Roble, Mohad Mohamed Hajji, Aden Hussein Ibrahim, Daud Abdullah Hassan, Hassan Hussein Mohamed, Adil Nur Ali, Mohamed Saleh Hussein, Jabril Hassan Mohamed, Sadag Abdugadir Mohamed na Dek Abdullah Nur.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BURUNDI YAILAZA SOMALIA 2-0 MACHAKOS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top