• HABARI MPYA

  Jumamosi, Novemba 30, 2013

  AZAM YAMPA MKATABA WA MIAKA MIWILI KOCHA WA AKINA ETO’O


  Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
  KLABU ya Azam leo imemtambulisha kocha wake mpya, Joseph Marius Omograia wa Cameroon iliyempa Mkataba wa miaka miwili kuanzia leo.
  Omog anatua Azam akitokea klabu ya A.C Leopards ya Kongo Brazavville ambayo aliiwezesha kutwaa ubingwa wa ligi ya nchi hiyo kwa misimu miwili mfululizo (2012 na 2013) na kumaliza ukame wa mataji wa miaka 30. 
  Mwenyekiti wa Azam FC, Sheikh Said Mohammad kulia akimtambulisha kocha mpya, Omog katikati leo

  Kwa mwaka huu wametwaa ubingwa wakiwaacha wapinzani wao, Diables Noirs kwa pengo la pointi kumi (10) wakikusanya pointi 87 katika ligi yenye timu 18.   
  Pia ni mwaka jana tu (2012) aliiwezesha A.C Leopards kunyakua ubingwa wa Kombe la Shirikisho la Afrika kwa kuzipiga kumbo timu ngumu na zenye uzoefu mkubwa kama vile Mas de Fes ya Morocco, Heartlands ya Nigeria na Sfaxien ya Tunisia.   
  Mafanikio hayo ya kutwaa ubingwa wa Afrika yalifikiwa baada ya miaka 38 tangu klabu ya Jamhuri yas Kongo ifanye hivyo, na kumfanya kocha Omog kuwa moja ya makocha wa kupigiwa mfano barani Afrika.
  Kadhalika mwaka huu 2013, A.C Leopards chini ya ukufunzi wa Omog ilitinga hatua ya makundi ya Ligi ya mabnigwa Afrika na kupangwa katika kundi moja na timu mbili zilizocheza fainali; Al Ahly ya Misiri (bingwa) na Orlando Pirates ya Afrika Kusini.
  Yote hayo ameyafanya akitumia asilimia kubwa ya wachezaji wa ndani ya Kongo huku akiwainua kutoka katika hali ya kuonekana wachezaji wa wastani hadi kuwa tishio na kuhofiwa kote barani Afrika.
  “Azam Football Club inamuona kocha Omog kuwa anakidhi vigezo vya kuendana na dira ya klabu ambayo ni kukuza na kuwaendeleza wachezaji na kushindana kwa kiwango cha juu kwa lengo la kuwa mabingwa katika mashindano mabalimbali ambayo timu inashiriki,”.
  “Uongozi wa Azam FC utampatia ushirikiano wa kutosha ili kufanikisha malengo na mipango thabiti ya klabu,”imesema taarifa ya Azam katika tovuti yao.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AZAM YAMPA MKATABA WA MIAKA MIWILI KOCHA WA AKINA ETO’O Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top