• HABARI MPYA

  Alhamisi, Novemba 28, 2013

  NGASSA: NIMEKUJA KUWASHIKA NAIROBI

  Na Mahmoud Zubeiry, Nairobi
  MRISHO Khalfan Ngassa, mshambuliaji tegemeo wa Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars amesema kwamba amekuja kikamilifu katika Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge mwaka huu na anataka kufanya kazi nzuri kuisaidia timu yake kubeba Kombe.
  Nimekuja kuwashika; Mrisho Ngassa amesema anataka kufanya kweli Challenge ya mwaka huu 

  Akizungumza na BIN ZUBEIRY jana, Ngassa alisema kwamba ameamua Challenge ya mwaka huu afanye kazi kweli ili kujenga heshima yake binafsi na kuisaidia timu.
  “Sikuja kutania hapa, najua haya mashindano ni magumu, lakini ninataka kufanya kazi, na nitafanya. Watanzania tu waniombbe dua ya uzima na nini, baada ya hapo wataona wenyewe,”alisema.
  Ngassa ameelezea kundi lao na kusema kwamba kuna upinzani mkali baina ya Burundi, Zambia na wao wakati Somalia amewashusha thamani akisema; “wasindikizaji hao”.
  “Hapa ushindani ni kati yetu na Zambia na Burundi, lakini Somalia kwa kweli sijui kama watafika popote,”alisema Ngassa.   
  Kili Stars inatarajiwa kuanza kampeni zake za kuwania taji la nne la Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge leo kwa kumenyana na Zambia Uwanja wa Machakos katika mchezo wa Kundi B utakaotanguliwa na mechi nyingine kati ya Somalia na Burundi.         
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NGASSA: NIMEKUJA KUWASHIKA NAIROBI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top