• HABARI MPYA

  Alhamisi, Novemba 28, 2013

  KILI STARS NA ZAMBIA WALIVYOCHIMBA NYASI ZA KENYATTA LEO, NA BURUNDI NA SOMALIA NAO...

  Mkombozi; Mfungaji wa bao la kusawazisha la Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars, Said Morad kushoto akishangilia na wenzake baada ya kufunga dhidi ya Zambia katika sare ya 1-1 Uwanja wa Kenyatta, mjini Machakos, Kenya leo katika mechi ya Kundi B, Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge.  

  Mshambuliaji wa Stars, Elias Maguri kushoto akimtoka beki wa Zambia, Bronson Chama kulia

  Kiungo wa Stars, Hassan Dilunga akimtoka mshambuliaji wa Zambia, Ronald Kampamba

  Mchezaji filamu na mwimbaji, Dokii ambaye kwa sasa anasoma Kenya alikuwepo Uwanja wa Kenyatta leo kuishangilia timu ya nyumbani, Stars

  Beki wa Stars, Erasto Nyoni akipiga krosi

  Kiungo wa Stars, Salum Abubakar 'Sure Boy' akimtoka kiungo wa Zambia, Kondwani Mtonga

  Elias Maguri akitafuta mbinu za kumtoka Bronson Chama

  Hassan Dilunga akipambana na kiungo wa Zambia, Rodrick Kabwe 

  Elias Maguri na Bronson Chama leo ilikuwa shughuli pevu

  Mshambuliaji wa Stars, Mrisho Ngassa akiwafunga tela mabeki wa Zambia

  Salum Abubakar 'Sure Boy' akimtesa kiungo wa Zambia, Stanley Nshimbi

  Kipa wa Zambia, Nsabata Toaster akidaka mpira mbele ya Elias Maguri, huku Bronson Chama akiwa tayari kumsaidia na Mrisho Ngassa anasubiri mpira upotee 

  Kiungo wa Zambia, Rodrick Kabwe akia amepitia mpira miguuni mwa Erasto Nyoni 

  Kikosi cha Stars leo

  Kikosi cha Zambia

  Kikosi cha Burundi kilichoifunga Somalia 2-0 katika mchezowa kwanza Kundi B mchana wa leo Uwanja wa Kenyatta

  Kikosi cha Somalia

  Somalia na Burundi

  Nahodha wa Burundi, Hakizimana Hassan akimtoka beki wa Somalia  

  Hata hivyo, jitihada za Hakizimana ziliishia mikononi mwa kipa wa Somalia, Mohamed Sherrif aliyedaka
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KILI STARS NA ZAMBIA WALIVYOCHIMBA NYASI ZA KENYATTA LEO, NA BURUNDI NA SOMALIA NAO... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top