• HABARI MPYA

    Tuesday, November 26, 2013

    MECHI YA TANZANITE SASA KUCHEZWA DAR

    Na Princess Asia, Dar es Salaam
    MECHI ya kwanza ya Raundi ya michuano ya Kombe la Dunia, Kanda ya Afrika kwa wanawake chini ya miaka 20 kati ya Tanzania (Tanzanite) na Afrika Kusini iliyokuwa ichezwe Mwanza sasa itafanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Baada ya ukaguzi uliofanywa na maofisa wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imebainika uwanja huo unatakiwa ufanyiwe marekebisho ambayo hayawezi kuwahi Desemba 7 mwaka huu, siku ambayo ndiyo mechi hiyo inatakiwa kuchezwa.
    Vyumba vya wachezaji vya Uwanja huo ndilo eneo ambalo linatakiwa  kufanyiwa marekebisho makubwa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MECHI YA TANZANITE SASA KUCHEZWA DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top