• HABARI MPYA

  Jumamosi, Novemba 23, 2013

  ENYEAMA ASHINDA TUZO UFARANSA

  AWABWAGA WAKALI KIBAO AKIWEMO IBRAHIMOVIC

  Vincent Enyeama

  KIPA wa Nigeria na OSC Lille Metropole, Vincent Enyeama, amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Oktoba wa Chama cha Wacheza wa Kulipwa Ufaransa (UNFP).

  Enyeama, ambaye aliidakia Nigeria ikikata tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia mwakani Brazil dhidi ya Ethiopia mwishoni mwa wiki iliyopita, amewapiku nyota kama Zlatan Ibrahimovic na Edinson Cavani kutwaa tuzo hiyo.
  Mzuia michomo huyo wa zamani wa Hapoel Tel Aviv, atakabidhiwa tuzo yake leo Jumapili wakati timu yake Lille, ikimenyana na Toulouse katika Ligue 1.
  Mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 31 ameorodheshwa pia katika orodha ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ya wachezaji wanaowania tuzo ya Mwanasoka Bora Afrikamwaka 2013.
  Amedaka mechi 11 bila kuruhusu nyavu zake kuguswa kati ya 13 za ligi na yuko kwenye nafasi ya kuipiku rekodi ya Salvatore Sirigu wa PSG kudaka dakika 948 bila kufungwa, hadi sasa akiwa ametimiza dakika 765 bila kufungwa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ENYEAMA ASHINDA TUZO UFARANSA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top