• HABARI MPYA

  Ijumaa, Novemba 29, 2013

  KIIZA NA NIYONZMA WAONYESHANA KAZI MACHAKOS

  Na Mahmoud Zubeiry Nairobi
  WACHEZAJI wawili wa Yanga SC, kiungo Haruna Niyonzima na mshambuliaji Hamisi Kiiz leo wanatarajiwa kuonyeshana kazi Uwanja wa Kenyatta, Machakos, Kenya.
  Hiyo ni katika mchezo wa Kundi C wa Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge baina ya timu zao, Uganda ya Kiiza na Rwanda na Niyonzima.
  Hamisi Kiiza ataiongoza Uganda dhidi ya Rwanda leo na chini ni Haruna Niyonzima wa Rwanda

  Mchezo huo utafanyika jioni na utatanguliwa na mchezo mwingine wa kundi hilo kati ya Sudan na Eritrea.
  Kiiza na Niyinzima wamekuwa wakifurahia mafanikio pamoja katika klabu ya Yanga, lakini leo watatengeneza tofauti kwa dakika 90 Uwanja wa Machakos kila mmoja kwa maslahi ya taifa lake.
  Raundi ya kwanza ya CECAFA Challenge inatarajiwa kukamilika leo kwa mechi hizo za Kundi C, baada ya juzi na jana kuchezwa mechi za Kundi A na B. je, ni Kiiza au Niyonzima ataipa ushindi timu yake leo? Bila shaka hilo ni jambo la kusubiri na kuona.   

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KIIZA NA NIYONZMA WAONYESHANA KAZI MACHAKOS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top