• HABARI MPYA

  Ijumaa, Novemba 22, 2013

  MBEYA CITY YAICHAPA AZAM, COASTAL YAITAMBIA JKT RUVU, HAO KAGERA SASA…

  Na Prince Akbar, Dar es Salaam
  MICHUANO ya Kombe la Uhai, inayohusisha vijana chini ya umri wa miaka 20, imeendelea leo kwenye viwanja vitatu mjini Dar es Salaam na Azam FC imechapwa bao 1-0 na Mbeya City, Uwanja wa DUCE asubuhi.
  Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam, Kagera Sugar imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Rhino Rangers, wakati Coastal Union imeifunga JKT Ruvu mabao 2-1.

  Mabao ya Kagera yamefungwa na John Chidi dakika za 40 na 77 na Shaaban Manafi dakika ya 45, wakati bao pekee la Rhino limefungwa na Laurent Ukungu dakika ya 24.
  Mabao ya Coastal yamefungwa na Mohamed Rajab dakika za 61 na 90, wakati la Ruvu lilifungwa na Anuar Suleiman.   Mchezo wa asubuhi Uwanja wa Karume, Prisons iliifunga 3-1 Mtibwa Sugar.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MBEYA CITY YAICHAPA AZAM, COASTAL YAITAMBIA JKT RUVU, HAO KAGERA SASA… Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top