• HABARI MPYA

  Jumanne, Novemba 26, 2013

  BARA KUJIFUA STIMA PAMOJA NA SUDAN, ETHIOPIA LEO

  Na Mahmoud Zubeiry, Nairobi
  TIMU zinazoshiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge ambayo mwaka inafanyika hapa Nairobi, Kenya ikidhaminiwa na Serikali, zitafanya mazoezi katika viwanja vijnne tofauti leo.    
  Viwanja hivyo ni Stima Club, Chuo Kikuu cha Strathmore, Uwanja wa City Stadium Ktuo cha Kimataifa cha Michezo cha Moi (MISC), Kasarani.
  Uchovu umeisha; Kocha wa Bara, Kim Poulsen leo atakiongoza kikosi chake mazoezini kwa mara ya kwanza Nairobi, baada ya kuwasili jana. Chini, kikosi cha Stars kikiwasili Nairobi jana usiku.

  MISC, Kasarani umetengwa maalum kwa ajili ya wenyeji, Kenya, Harambee Stars, wakati Tanzania Bara, Sudan na Ethiopia watafanya pamoja kwenye Uwanja wa Stima.
  Rwanda, Sudan Kusini na Burundi watatumia viwanja viwili vya Strathmore, huku Somalia, Zanzibar na Eritrea wakitumia mwingine na mabingwa watezi Uganda na Zambia watatumia Uwanja wa City.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BARA KUJIFUA STIMA PAMOJA NA SUDAN, ETHIOPIA LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top