• HABARI MPYA

    Wednesday, November 27, 2013

    MAN UNITED WAPATA MSUKOSUKO ANGANI WAKITAKA KUTUA UWANJA WA NDEGE WA COLOGNE

    KOCHA David Moyes na kikosi chake cha Manchester United walipatwa na mshituko wakiwa angani Ujerumani jana kwa safari ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Bayer Leverkusen baada ya ndege hiyo kughairi kutua Uwanja wa Ndege wa Cologne.
    Ndege ya United ilikuwa umbali wa mita 400 kuelekea chini Uwanja wa Ndege wa Cologne wakati Rubani alipofoka akisema kuna ndege nyingine katika eneo alilotaka kutua.
    Wakati wachezaji wa klabu hiyo ya Ligi Kuu ya England wakirejea kwenye siti zao, Rubani akalazimika kuzunguka upande mwingine kuishusha ndege hiyo
    Wametulia: Ashley Young na Jonny Evans wakiwa Uwanja wa ndege wa Manchester kabla ya safari ya Ujerumani
    Hairy moment: Rio Ferdinand tweeted that he had 'just recovered from a choppy landing'
    Rio Ferdinand ametweet juu ya kutua kwao salama
    David Moyes
    Wayne Rooney
    David Moyes na Wayne Rooney Uwanja wa Ndege wa Manchester

    Kikosi kizima cha United, wakiwemo wachezaji, kocha David Moyes na viongozi wote wa benchi la Ufundi walikuwa kwenye ndege na beki Rio Ferdinand akatweet baada ya kutua: "Tumetua Ujerumani...baada ya kupatwa msukosuko hivi wakati wa kutua.’
    Sir Bobby Charlton, ambaye alikuwepo katika msafara wa United uliopata ajali mjini Munich mwaka 1958, na Sir Alex Ferguson hawakuwamo kwenye ndege hiyo
    All smiles: David Moyes was happy enough when he gave a press conference in Germany
    David Moyes alikuwa mwenye furaha kiasi cha kutosha baada ya kutua Ujerumani wakati anazungumza na Wandishi wa Habari
    Cheery: Chris Smalling was also in buoyant mood despite the air scare
    Chris Smalling alikuwa kwenye hali nzuri pia
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAN UNITED WAPATA MSUKOSUKO ANGANI WAKITAKA KUTUA UWANJA WA NDEGE WA COLOGNE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top